1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaLibya

12 wahukumiwa athari za mafuriko ya Derna, Libya

29 Julai 2024

Watu 12 wametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo jela kutokana na dhima yao katika janga la mafuriko lililoukumba mji wa mashiriki mwa Libya wa Derna mwaka uliopita.

https://p.dw.com/p/4iqHy
Athari za mafuriko yaliyoikumba Derna, Libya mwaka 2023.
Uharibifu uliotokana na mafuriko na kupasuka kwa mabwawa makubwa ya maji kwenye mji wa Derna nchini Libya. Picha: Halil Fidan//AA/picture alliance

Mkasa huo ulisababisha vifo vya maelfu ya watu. Ofisi ya mwandesha mashtaka wa Libya imesema watuhumiwa hao ambao wanajumuisha wafanyakazi wa serikali na maafisa wa serikali za mitaa wametiwa hatiani kutokana na majukumu yao ya kusimamia mabwawa makubwa ya maji.

Wamehukumiwa kifungo cha kati ya miaka 9 hadi 27 gerezani kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa kusimamia mabwawa ya nchi hiyo ambayo mawili yalipasuka na kusababisha mafuriko ya kutisha.

Mnamo Septemba 10 mwaka jana,  kimbunga Daniel kiliipiga pwani ya mashariki mwa Libya na kusababisha mafuriko na kupasuka kwa mabwawa makubwa mawili yaliyosomba karibumji mzima wa Derna.

Zaidi ya watu 4,300 walikufa na maelfu wengi hadi leo hawajulikani walipo.