Uingereza inawasaka washukiwa wa shambulizi lililotokea katika stesheni ya treni ya chini ya ardhi, ambalo limesababisha kujeruhiwa kwa zaidi ya watu 20. Na Ujerumani inataka kuiongezea Uturuki mbinyo wa kiuchumi kwa lengo la kufanikisha kuachiwa huru kwa raia wa Ujerumani ambao wapo kizuzini nchini humo.