2022: Mwaka wa kufikwa na mabadiliko ya tabia nchi
Mwaka huu kumeshuhudiwa joto kali, ukame, majanga ya moto, dhoruba kali na mafuriko kote ulimwenguni yanayohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi. Tazama yaliotokea kwa mwaka huo.
Ulaya: Joto na ukame kuliko siku za nyuma
Majira ya joto ya Ulaya yalishuhudia joto kali na ukame mbaya zaidi katika miaka 500. Zaidi ya watu 500 walikufa kutokana na joto nchini Uhispania huku kiwango cha joto kikifikia nyuzi joto 45. Nchini Uingereza, joto lilipindukia nyuzi 40. Maeneo mengine ya mabara kulikuwa na ukame zaidi, maeneo mengi yalikuwa na shida ya maji.
Moto wa msituni ulizagaa Ulaya yote
Kuanzia Ureno, Uhispania na Ufaransa hadi Italia, Ugiriki, Cyprus na Siberia kwa upande wa Kaskazini, bara hilo liliwaka moto. Moto umeteketeza hekta 660,000 ikiwa sawa na eka 1,630,896) za ardhi hadi katikati ya mwaka - ni kubwa zaidi tangu kuanza kuwekwa rekodi 2006.
Janga la mafuriko Asia
Mvua kubwa za masika ziliikumba Pakistan,na kuzamisha theluthi ya taifa eneo la nchi. Mafuriko hayo yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 1100, kuacha wengine milioni 33 bila makazi na kusababisha kuenea kwa magonjwa. Hali kama hiyo iliikumba Afghanistan. Mafuriko hayo yaliharibu maelfu ya hekta za ardhi, na hivyo kuzidisha njaa kali nchini humo.
Joto kali na vimbunga vinakumba bara hilo pia
Kabla ya mafuriko, Afghanistan, Pakistan na India zilikumbwa na joto kali na ukame. China, wakati huo huo ilikumbana na ukame wake mbaya zaidi katika miaka 60 na joto kali. Kufikia msimu wa vuli vimbunga 12 tayari vilikuwa vimepiga nchini humo. Dhoruba kubwa pia ilipiga Ufilipino, Japan, Korea Kusini na Bangladesh. Mabadiliko ya hali ya tabia nchi yanafanya dhoruba kama hizo kuwa na nguvu zaidi.
Madhara ya makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi Afrika
Afrika ipo katika joto kali na kwa kasi zaidi kuliko kuliko mabara mengine. Hali hiyo inasababisha maafa makubwa kutokana na mabadiliko ya unyeshaji wa mvua, ukame na mafuriko. Somalia inakabiliana na ukame mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 40. Mgogoro huo umewalazimu zaidi ya watu milioni moja kuyahama makazi.
Uhamiaji na njaa katika bara la Afrika
Mafuriko na ukame mkubwa umefanya kilimo na ufugaji kutowezekana katika sehemu fulani za Afrika. Kwa hivyo, mamilioni ya watu wanakabiliwa na Wengi hadi sasa tayari wamepoteza maisha kwa njaa hiyo nchini Ethiopia, Somalia na Kenya.
Moto na mafuriko huko Amerika Kaskazini
Dhoruba kali zilikumba majimbo ya Marekani ya California, Nevada na Arizona. Janga la moto liliyaunguza majimbo yote matatu katika halijoto ya zaidi ya nyuzi 40 C mwishoni mwa msimu wa kiangazi. Kinyume chake, mvua kubwa iliyonyesha mapema wakati wa kiangazi ilisababisha mafuriko makubwa katika Mbuga ya Kitaifa ya Yellowstone, pamoja na Kentucky.
Vimbunga vimeivuruga Marekani
Mwezi Septemba, Kimbunga Ian kililiharibu jimbo la Florida. Mamlaka za eneo hilo zilielezea uharibifu huo kama "wa kihistoria" kwa ukubwa. Hapo awali Ian kilishambulia Cuba, ambapo wakazi walikosa umeme kwa siku kadhaa. Fiona kimekuwa kimbunga kibaya zaidi cha kitropiki kuwahi kuipiga Canada baada ya awali kuyaathiri maeneo ya Amerika ya Kusini na Carribean.
Dhoruba mbaya za kitropiki huko Amerika ya Kati
Fiona haikuwa dhoruba pekee iliyopiga Amerika ya Kati. Mnamo Oktoba, Kimbunga Julia kilipiga Colombia, Venezuela, Nicaragua, Honduras na El Salvador, na kusababisha uharibifu mkubwa. Kuongeza joto duniani kunaongeza halijoto baharini, jambo ambalo linasababisha hali mbaya ya vimbunga.
Ukame mkubwa Amerika ya Kusini
Ukame unaoendelea kukumba karibu bara zima la Amerika Kusini. Chile, kwa mfano, imekuwa ikikabiliwa na ukosefu wa mvua uliokithiri tangu 2007. Katika mikoa mingi, vijito na mito imepungua kwa kati ya 50 na 90%. Mexico haijapata mvua kwa miaka kadhaa mfululizo. Argentina, Brazil, Uruguay, Bolivia, Panama na sehemu za Ecuador na Colombia pia wanaishi na ukame.
Mafuriko New Zealand na Australia
Mvua kubwa ilisababisha mafuriko makubwa Australia mara kadhaa 2022. Kati ya Januari na Machi, pwani ya mashariki ya nchi ilifikwa na takriban kiwango cha sawa na inachopata Ujerumani kwa mwaka mmoja. New Zealand haikuepuka mafuriko.