1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

70% ya waliouawa ukanda wa Gaza ni wanawake na watoto

8 Novemba 2024

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema leo kuwa takriban asilimia 70 ya watu waliouawa vitani katika ukanda wa Gaza ni wanawake na watoto.

https://p.dw.com/p/4moDu
Vita vya Gaza
Vita vya GazaPicha: Bashar Taleb/AFP

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imesema leo kuwa takriban asilimia 70 ya watu waliouawa vitani katika ukanda wa Gaza ni wanawake na watoto na kulaani kile ilichokitaja kuwa ukiukaji wa kanuni za msingi za sheria ya kibinadamu ya kimataifa.

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja huo wa Mataifa Volker Türk, amesema ni muhimu kuwa na takwimu zinazofaa kuhusiana na madai ya ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa kupitia vyombo vya mahakama vinavyoaminika na visivyokuwa na upendeleo na kwamba, taarifa zote muhimu na ushahidi zinakusanywa na kuhifadhiwa.

Hata hivyo ofisi ya waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, haikutoa tamko la mara moja kuhusiana na ufichuzi huo ilipotakiwa kufanya hivyo na shirika la habari la Reuters.