1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abiy asema "hana nia" ya kuingia vitani na Somalia

6 Februari 2024

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameondoa wasiwasi wa kutokea vita kati ya nchi yake na Somalia.

https://p.dw.com/p/4c6Th
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy AhmedPicha: Fana Broadcasting Corporate S.C.

Wasiwasi huo ulikuwepo baada ya mzozo kuibuka hivi karibuni kufuatia makubaliano kati ya Addis Ababa na Somaliland yaliyoipa nafasi Ethiopia kutumia  bahari ya Sham.

Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud aliwahi kusema hivi karibuni kwamba yuko tayari kuingia vitani na Ethiopia, kuizuia nchi hiyo kujenga bandari katika ardhi yake.

Akihutubia wabunge leo, Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema "hana nia" ya kuingia vitani na Somalia.

Amesema Ethiopia na Somalia ni ndugu na kwamba maendeleo ya nchi hiyo ni sawa na maendeleo ya Ethiopia.

Ameeleza kuwa, maelfu ya Waethiopia wamekufa nchini Somalia ili kuhakikisha amani ya taifa hilo la pembe ya Afrika, akimaanisha mchango wa wanajeshi wa Ethiopia ndani ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika unaokabiliana na kundi la kigaidi la Al-Shabab.

Ethiopia ilitia saini mkataba wa makubaliano na jimbo lililojitenga la Somaliland mnamo Januari mosi. Hati ya makubaliano hayo haijawekwa hadharani kwa umma japo Somaliland imesema Ethiopia imekubali kuitambia Somaliland kama taifa huru.

Makubaliano hayo yameikasirisha Somalia ambayo inadai kuwa jimbo la Somaliland ni sehemu ya himaya yake.