1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABU DHABI: Schroeder akamalisha ziara ya Ghuba

5 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZN

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameikamilisha ziara yake ya wiki moja katika nchi za Ghuba kwa kutua Abu Dhabi,Umoja wa Falme za Kiarabu.Schroeder amekubali kuimarisha mchango wa Ujerumani katika ujenzi mpya wa Iraq na vile vile kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Kiiraqi nchini Umoja wa Falme za Kiarabu.Mjini Abu Dhabi Schroeder alishuhudia kandarasi nane za biashara zikitiwa saini kati ya Ujerumani na Umoja wa Falme za Kiarabu kwa miradi mbali mbali yenye thamani ya Euro bilioni moja.Miongoni mwa kandarasi hizo ni makubaliano ya kulipatia jeshi la Umoja wa Falme za Kiarabu vifaru 32 aina ya Fuchs.Baadae hii leo Kansela Schroeder anarejea Ujerumani.