1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABU DHABI: Ziara ya Schroeder nchi za Ghuba

6 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZG

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani amemaliza ziara yake ya wiki moja katika nchi za Ghuba kwa maridhio.Alipokuwa katika kituo chake cha mwisho nchini Umoja wa Falme za Kiarabu,Schroeder alisema majadiliano yake pamoja na maafisa wa serikali na biashara katika nchi saba za Mashariki ya Kati yalikuwa na mafanikio makubwa mno.Kuhusu uwezekano wa Ujerumani kuziuzia silaha nchi za Ghuba,Kansela Schroeder amesema maombi hayo yatafikiriwa kwa kuizingatia kila nchi peke yake na kuambatana na sheria za Ujerumani kuhusika na usafirishaji wa bidhaa nje ya nchi.Wakati wa ziara yake Schroeder vile vile alitia saini makubaliano ya kuimarisha mchango wa Ujerumani kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Kiiraqi nchini Umoja wa Falme za Kiarabu ili kuisaidia serikali ya mpito ya Iraq iliyochaguliwa hivi karibuni.