1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACCRA:Viongozi wa AU watathmini kuundwa kwa Muungano wa Afrika

2 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmT

Viongozi wa Umoja wa Afrika wanaokutana mjini Accra nchini Ghana wanajadilia mipango ya kuwa na Muungano wa Mataifa ya Afrika ulio na lengo la kuondoa suala la mipaka baina ya mataifa.Hiyo ndiyo mada rasmi katika ajenda ya mkutano huo ulioingia siku yake ya pili.Pembezoni mwa suala hilo viongozi hao aidha wanatarajia kujadilia matatizo yanayoyumbisha Bara la Afrika hususan eneo la Darfur na Zimbabwe.

Rais wa Libya Muamer Kadhafi anapigia debe hoja ya kuundwa kwa Muungano wa bara la Afrika ili kuimarisha umoja.

Kauli hiyo inapingwa na Rais mpya wa Nigeria Umaru YarAdua anayependekeza kuimarishwa kwa taasisi zilizopo badala ya mabadiliko mapya.

Naibu Katibu Mkuu wa Umoaj wa Mataifa Asha Rose Migiro alisema kuwa matatizo ya Somalia yasiachiwe bara la Afrika pekee huku Umoja wa Mataifa unaunga mkono ushirikiano zaidi katika mataifa ya Afrika.

Maandamano yamepigwa marufuku hadi siku ya mwisho ya kikao hicho cha siku tatu.Polisi alfu mbili wanashika doria mjini humo.