Afrika kuanza kutumia satalaiti kwa mazingira, tabianchi
13 Agosti 2019Kampuni ya Dijitali ya Afrika iko tayari kutoa huduma hiyo kote barani humo kwa kutumia njia ya satalaiti kukusanya habari zitakazoyasaidia mataifa, mashirika na wadau binafsi kufanya maamuzi kuhusu masuala ya mazingira. Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Adam Lewis, alisema kuwa mpango huo utakkuwa "ngazi nzuri ya kubadilisha miundombinu na raslimali za Afrika, kwani utaunganisha data, kilimo, uhifadhi na uvumbuzi.”
“Moja ya umuhimu wa data ni kwamba hutusaidia ni kuokoa muda na hata raslimali iwe ni nguvu-kazi ama raslmali za kiuchumi. Pia hutusaidia kutokupoteza wakati.” Alisema Waziri wa Ulinzi wa Kenya, Rachel Onamo, kwenye mkutano wa siku ya kidijitali barani Afrika uliofanyika Nairobi.
Sayansi huyasaidia mataifa barani Afrika kupunguza gharama za kuchanganua data, hasa katika kukabiliana na changamoto zinazoyakabili ili kutimiza Malengo ya Maendeleo Endelevu yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa.
Sierra Leone yaongoza njia
Tayari Sierra Leone inatumia data kutoka kwenye satalaiti inapotekeleza ajenda hizo za Maendeleo Endelevu.
"Tunahitaji kushirikiana ili kuboresha mahusiano yetu ili kuhakikisha yanadumu kwa kipindi kirefu, na kusaidiana data na maelezo muhimu. Hilo litatusaidia kufikia ajenda ya mwaka 2030 ya malengo ya maendeleo endelevu, na ajenda ya mwaka 2063. Zote zinaegemea mahusiano dhabiti na marafiki kama vile kampuni ya Dijitali ya Afrika," alisema Mamadi Gebeh, naibu waziri wa habari na mawasiliano wa Sierra Leone, ambaye pia alishiriki mkutano huo wa London.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uchunguzi na Tathmini wa Ghana, William Kwasi, alisema watunga sera na wabunge wanastahili kuhusishwa kwenye mpango huu ili wafahamu utendajikazi wake. Mkurugenzi wa kampuni ya Dijitali ya Afrika daktari Adam Lewis amepongeza mradi wenyewe.
Baadaye afisi ya mpango huu uunaofadhiliwa na serikali ya Australia itafunguliwa jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Shisia Wasilwa/DW Nairobi