Afya ya uzazi bado ni changamoto kwa mataifa mbalimbali
11 Novemba 2022Wito huo umetolewa na viongozi mbali mbali wakiongozwa na Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Kikwete katika uzinduzi wa ripoti hiyo maalumu, juu ya utekelezaji wa maazimio ya Nairobi yaliyowekwa mwaka 2019 ambapo maazimio 12 yalionekana ndio muhimu zaidi na yanahitaji utekelezaji.
Akizungumza katika mkutano huo Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi ambaye alikuwa mweyeji wa mkutano alisema kwa msaada wa washirika wa maendeleo Serikali yake inaendelea kuandaa mfumo wa afya, kujenga miundo mbinu ya Afya , kuajiri rasilimali watu, sambamba na kupata vifaa tiba zaidi za afya ili kutoa huduma bora za afya mijini na vijijini.
Kamisheni ya ufuatiliaji wa maazimio ya Nairobi yenye makamishna 27 na wenyeviti wenza wawili Jakaya Kikwete na Michaelle Jeans. Kazi ya kamisheni hiyo imechukua miaka mitatu kufuatilia utekelezaji wa kazi hiyo.