1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Al-Burhan aelekea New York kwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa

21 Septemba 2023

Mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, ambaye yumo vitani kwa miezi kadhaa na wanamgambo wa RSF, ameondoka kuelekea mjini New York ambako anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4WdCR
Sudan | General Abdel Fattah Al-Burhan
Picha: Sudanese Army/AFP

Katika wiki za hivi karibuni, Al-Burhan amekuwa akifanya ziara kadhaa nje ya nchi baada ya kuhamisha ngome yake kutoka mji mkuu Khartoum hadi Port Sudan. 

Burhan tayari ametembelea Misri, Sudan Kusini, Qatar, Eritrea, Uturuki na Uganda. 

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan ziarani nchini Uganda

Wachambuzi wanasema kuwa harakati zake za kidiplomasia zinalenga kuimarisha uhalali wake endapo kutakuwa na mazungumzo ya kusitisha mapigano. 

Mzozo wa Sudan ulioibuka Aprili 15 mwaka huu tayari umesababisha vifo vya takriban watu 7,500, na kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya watu milioni tano wameyakimbia makazi yao.