Albino au Zeruzeru: Namna ya kujitazama
11 Januari 2007Hali ya zeruzeru hutokea ikiwa kuna historia ya hali hiyo katika familia. Hali ya Albino inatokea kwa aina mbili katika binadam: ukosefu wa chembechembe za rangi kwenye ngozi,macho na nywele au ukosefu wa rangi kwenye macho pekee. Katika aina hiyo ya pili nywele na ngozi zinakuwa na rangi ya kawaida. Aina ya kwanza aghalabu huonekana zaidi.
Hali hii inatokana na hitilafu katika shanga za urathi na ni tatizo la kurithi.Albino aghalabu wana matatizo ya macho: hawaoni mbali au hawaoni karibu japo miwani huweza kusaidia tatizo hilo.Wengine wanapata tatizo la macho kupesapesa bila hiari vilevile kuathiriwa na mwangaza.H ali hiyo hutokea hata katika wanyama na husababisha matatizo makubwa hasa katika wanyama wanaowinda.Matatizo ya macho na ukosefu wa rangi ya ngozi yanachangia kwa kiasi kikubwa.
Sikiliza kipindi kizima cha afya.