1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Scotland Sturgeon akamatwa

11 Juni 2023

Aliyekuwa Waziri Kiongozi wa Scotland Nicola Sturgeon amekamatwa leo na polisi inayochunguza fedha za chama tawala kinachounga mkono uhuru wa nchi hiyo, cha Scottish National - SNP

https://p.dw.com/p/4SRmL
England Schottland Glasgow | Nicola Sturgeon verhaftet
Picha: ANDY BUCHANAN/AFP/Getty Images

Polisi ya Scotland imesema mwanamke mwenye umri wa miaka 52 alikamatwa kama mshukiwa katika uchunguzi wa ufadhili na fedha za chama hicho.

Soma pia: Bunge la Scotland lamthibitisha Yousaf kuwa Waziri kiongozi

Polisi nchini Uingereza haitaji majina ya washukiwa hadi watakaposhitakiwa. Shirika la habari la BBC na vyombo vingine vilimtambua mwanamke huyo kuwa ni Sturgeon.

Wapelelezi wamesema wanachunguza jinsi pauni 600,000 zilizotengewa kampeni za uhuru wa Scotland zilivyotumiwa.

Sturgeon alijiuzulu ghafla Februari mwaka huu baada ya miaka minane ya uongozi wa chama cha Scottish National na Waziri kiongozi wa serikali ya Scotland yenye madaraka ya ndani.