Asili na mazingiraBotswana
Almasi ya pili kwa ukubwa ulimwenguni yapatikana Botswana
23 Agosti 2024Matangazo
Kampuni hiyo imesema almasi hiyo iligunduliwa na kuchimbuliwa kwa kutumia kteknolojia ya Mega Diamond Recovery X-Ray.
Kampuni ya Lucara Diamond Corp haikutoa makadirio ya thamani ya almasi hiyo au kutoa maoni kuhusu ubora wake.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo nchini humo, Naseem Lahri, aliiwasilisha jiwe hilo, katika ofisi ya Rais Mokgweetsi Masisi jana Alhamisi.
Botswana ni moja ya mataifa yanayochimba zaidi madini ya almasi ambayo ndiyo chanzo kikubwa cha pato la taifa.
Kulingana na takwimu za Shirika la Fedha Duniani, madini hayo yanachangia asilimia 30 ya Pato la Taifa na asilimia 80 ya mauzo nje ya nchi.