1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Amman: Benki ya Dunia inatoa mkopo kwa Iraq

19 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEt5

Benki ya Dunia, kwa mara ya kwanza tangu kupita zaidi ya miaka 30, itaipa Iraq mkopo. Imetangazwa katika mkutano wa wafadhili huko Jordan kwamba benki hiyo itaikopesha Iraq dola milioni 500 kugharimia miradi ya miundo mbinu. Serekali ya Iraq imetoa mwito wa haraka kutaka nchi hiyo isaidiwe, na hadi sasa ni sehemu tu ya misaada ilioahidiwa kupewa ndio iliofika huko Baghdad. Pia leo mjini Munich hapa Ujerumani unaanza mkutano wa pili wa kiuchumi baina ya Ujerumani na Iraq. Mawaziri kadhaa wa Iraq watashiriki katika mkutano huu ambao utazungumzia nafasi ya makampuni ya Kijerumani kufanya biashara huko Iraq.