Angela Merkel atajishughulisha na nini baada ya kustaafu?
2 Desemba 2021Kama kansela amebaki ofisini kwa muda baada ya uchaguzi wa bunge, kama ilivyo desturi wakati serikali inapobadilika, mpaka serikali mpya inapochukua madaraka. Wakati huu wa kupika unatarajiwa hivi karibuni na Merkel atakamilisha rasmi kipindi cha miaka 16 kama mkuu wa serikali. Siku chache tu kuliko mlezi wake kansela wa zamani Helmut Kohl ambaye aliondoka afisini mwaka 1998 baada ya siku 5870.
Katika wiki za hivi karibuni Merkel amefanya vitu kwa mara ya mwisho; kukaa upande wa serikali katika bunge la Bundestag, kuongoza kikao cha mawaziri au kuongoza mkutano wa dharura kuhusu janga la corona na mawaziri wakuu wa majimbo yote 16 ya Ujerumani. Alhamisi jeshi la Ujerumani Bundeswehr lilimtunukia heshima kubwa na hafla ya kumuaga.
Mara ya mwisho Paris, London, Washington
Angela Merkel pia ameitembelea miji mingi mikuu ya dunia katika wiki za hivi karibuni kwa mara ya mwisho kama kansela. Wakati waziri mkuu wa Italia Mario Draghi aliposema kwenye mkutano wa kilele wa G20 kwamba anatumai kumuona Merkel mara kwa mara nchini Italia siku za usoni, Merkel alijibu akisema atakuwa na fursa ya kuishi maisha yake ya mahaba na Italia katika hali tofauti kabisa atakapoondoka afisi ya ukansela.
Merkel anaondoka afisni lakini atabaki kuwa bi Kansela katika hali rasmi ya utambulisho. Atakapozungumziwa au kuandikwa habari zake, atakuwa kansela mstaafu au kansela wa zamani.
"Tusubiri tuone nitakakojitokeza".
Siku ya kwanza kama kansela wa zamani huashiria mwanzo wa maisha mapya kwa Angela Merkel. Mpaka sasa amekaa kimya kuhusu atakachokifanya. Mnamo Julai wakati alipokuwa ziarani mjini Washington, Marekani kupokea tuzo ya heshima, alisema angependa kupumzika na kutokubali mialiko. Kwanza angetaka kutambua kwamba majukumu yake ya zamani yanafanywa na mtu mwingine lakini akaongeza kuwa anadhani atayafurahia maisha yake mapya.
Katika muda wake alisema anataka sana kutafakari kuhusu kinachompendeza. Amekuwa na muda mchache sana kufanya hivyo katika miaka 16 iliyopita. Baada ya hapo atasoma vitabu na macho yake atayafunga maana amechoka, atalala kidogo na kisha tutaona ni wapi atakakojitokeza.
"Bi Merkel" achunguzwa
Mpiga picha mmoja na mwandishi wa vitabu kuhusu uhalifu tayari wana mpango wa siku za usoni. Andreas Mühe amempiga picha kansela Merkel katika muonekano tofauti, hata akiwa mpweke, na kufanya maonyesho kutumia picha hizo. Mwandishi wa vitabu David Safier, kwa upande mwingine,anachukulia kansela Merkel kwa haraka atachoka na kusinywa bila kuwa na ratiba yake aliyoizowea, ambayo imesheheni mikutano na shughuli nyingi.
Katika kitabu chake chenye ucheshi "Miss Merkel" mwandishi huyo anamueleza kansela akikubaliana na taifa tulivu baada ya kuhamia nyumba yake ya zamani ya likizo huko Brandeburg. Kutembea na kuoka keki tu? Kwa kuzingatia filamu za kusisimua za Muingereza Miss Marple na Agatha Christie, Safier anamueleza Merkel akigundua kesi ya mauaj na kuichunguza kwa bidii kubwa.
Malipo yake ya uzeeni yako salama
Ni hadithi ya kubuni yenye kusisimua lakini swali la kwanza ambalo ni la msingi: Je mtu aliyepangiwa ratiba kutoka asubuhi had usiku kwa miongo kadhaa na ambaye amebeba jukumu kubwa, anaweza kusahau haraka kwa usiku mmoja? Unachokosa, kawaida unatambua kama hunacho tena, ameelezea kansela huyo mstaafu.
Angela Merkel alifikisha umri wa miaka 67 mnamo Julai 17. Kifedha hana haja ya kuwa na wasiwasi. Kwa sasa anapokea euro 25,000 kila mwezi kama kansela. Analipwa pia euro 10,000 kama mbunge katika bunge la Bundestag, ambalo amelihudumia kwa zaidi ya miaka 30. Merkel anapoacha kufanya kazi, kwanza ataendelea kupokea mshahara wake kwa miezi mitatu na baadaye atakuwa akilipwa nusu ya mshahara huo kama marupurupu kwa jumla ya miezi 21.
Kazi ya pili inawezekana
Wafanyakazi wastaafu wa serikali wanafungwa na sheria ya usiri. Lakini kama hawaruhusiwi kuzungumza, wanakuwa maarufu katika sekta ya biashara. Kama washauri na kwa sababu ya mawasiliano yao makubwa ya kisiasa. Baadhi ya watangulizi wa Merkel walijitosa katika biashara. Helmut Schmidt likuwa mhariri wa gazeti la kila wiki la "Die Zeit" mnamo 1982 na akawa mtoaji hotuba mashuhuri. Katika mahojiano ya mwaka 2021, kansela huyo wa zamani alisema aliifanya kuwa sheria kutotoa hotuba kwa malipo ya chini ya dola 15,000.
Kwa ufanisi mkubwa kuliko Helmut Schmidt, makansela wa zamani Helmut Kohl na Gerhard Schöder walifaulu sana kubadilisha historia zao za kisiasa kuwa ufanisi mkubwa kifedha. Kohl aliasisi kampuni ya kutoa ushauri wa kisiasa na masuala ya kimkakati, iliyomsaidia kupata fedha nyingi kama mshawishi na mtaalamu wa ushauri.
Makazi ya mjini Berlin
Je Angela Merkel anapania kuwa na ajira mpya au nafasi ya heshima? Hakuna kinacoifahamika kuhusu hilo. Kilicho wazi ni kwamba ataendelea kubaki mjini Berlin kwa wakati huu. Mume wake, mtaalamu wa kemia, Joachim Sauer, hajafikiria kuhusu kuwacha taaluma yake. Ingawa ni profesa katika chuo kikuu cha Humboldt mjini Berlin, mtaalumu huyo mwenye umwi wa miaka 72 amerefusha mkataba wake kama mtafiti mwandamizi wa cheo cha juu kwa sasa hadi 2022.
LINK: /dw/a-58886526