ANKARA: Erdogan aonywa asigombee urais
14 Aprili 2007Matangazo
Zaidi ya waandamanaji elfu 20 wamefanya maandamano kumuonya waziri mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan dhidi ya kugombea kiti cha urais katika uchaguzi wa mwezi ujao nchini Uturuki.
Waandamanaji hao walipeperusha vibendera vyekundu na kuimba nyimbo za kuupinga uislamu.
Waandamanaji hao wanahofia kuwa iwapo Erdogan atashinda katika uchaguzi huo basi huenda akapitisha sharia za kiislamu nchini humo.
Ingawa Uturuki haitawaliwi kwa misingi ya dini ya kiislamu lakini dini kuu nchini humo ni ya kiislamu.