1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA: Hakuna maafikiano kuhusu waasi wa Kikurd

27 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7CM

Maafisa wa Uturuki na Irak wamesema,hawana mpango wa kukutana kwa majadiliano zaidi kuhusu waasi wa Kikurd wanaoishambulia Uturuki kutoka kaskazini ya Irak.Ujumbe wa Irak ulikwenda Uturuki kujaribu kupata makubaliano juu ya njia za kukabiliiana na waasi wa Kikurd walio na vituo vyao kaskazini mwa Irak.

Uturuki imekataa mapendekezo yaliyotolewa na Irak ikisema,hatua zilizopendekezwa hazitoshi na zitachukua muda mrefu kabla ya kuleta matokeo yanayotakiwa.Serikali ya Uturuki itaamua hatua gani ichukuliwe dhidi ya waasi hao wa Kikurd, baada ya kufanywa ziara ya waziri mkuu Erdogan nchini Marekani mapema mwezi Novemba.