1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ankara. Iran na umoja wa Ulaya wakutana.

26 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC71

Kiongozi mkuu wa majadiliano ya kinuklia wa Iran amesema kuwa anatarajia kuwa jumuiya ya kimataifa itawasilisha kwa nchi yake mawazo mapya yenye lengo la kumaliza mkwamo wa kidiplomasia kuhusiana na mpango wa nchi yake wa kinuklia.

Ali Larijani alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Uturuki , Ankara, ambako yeye pamoja na mratibu wa sera za kigeni wa umoja wa Ulaya , Javier Solana , wanakutana kwa mazungumzo ya mwanzo yatakayochukua muda wa siku mbili.

Solana amesema kuwa anamatumaini wanaweza kupiga hatua za kutosha ili kuweka msingi kwa ajili ya majadiliano kamili muda mfupi ujao.

Wadadisi hata hivyo wanasema kuwa pande hizo mbili zinabaki kuwa mbali.

Mataifa mengi ya magharibi yanahofia kuwa Iran inaweza kutengeneza silaha la kinuklia.

Iran inasisitiza kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa ajili ya matumizui ya amani.