Ankara. Mkuu wa jeshi ataka Wakurd washambuliwe.
13 Aprili 2007Mkuu wa jeshi la Uturuki Jenerali Yasar Büyükanit amewaambia amesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa inatoa wito wa kufanyika mashambulio ya kijeshi ndani ya jimbo la kaskazini nchini Iraq ili kuwatafuta waasi wa Kikurd kutoka Uturuki.
Ameongeza kuwa hatua hiyo inahitaji kupata idhinisho la bunge, lakini amesisitiza kuwa majeshi ya ulinzi yako tayari kufanya operesheni hiyo. Pia ameeleza kuhusu taarifa za kijasusi kuwa waasi wanapanga mapambano mapya mwezi wa May.
Uturuki inawashutumu Wakurd wa Iraq kwa kuwaridhia na kuwaunga mkono waasi wa chama cha wafanyakazi wa Kurdistan, ambacho kimekuwa katika mapambano na Uturuki wakitaka kujitenga kwa jimbo lao lililoko kusini mashariki ya nchi hiyo tangu mwaka 1984.
Kiasi cha watu 37,000 wameuwawa katika mzozo huo.