ANKARA: Mshukiwa ugaidi akamatwa nchini Uturuki
7 Novemba 2007Matangazo
Polisi nchini Uturuki wamemkamata Mjerumani mwenye asili ya Kituruki,anaeshukiwa kulipatia miripuko kundi la Kiislamu lililokuwa na njama ya kushambulia vituo vya Marekani nchini Ujerumani. Inaaminiwa kuwa mshukiwa huyo alikimbilia Uturuki baada ya washirika wenzake watatu kukamatwa na polisi Septemba 4 nchini Ujerumani.