1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ANKARA : Schroeder ziarani Uturuki

4 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFGx

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameanza ziara yake nchini Uturuki ambapo anatarajiwa kumshinikiza Waziri Mkuu wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan kuongeza maradufu jitihada za mageuzi kabla ya kufanyika hapo mwezi wa Oktoba kwa mazungumzo juu ya nchi hiyo kujiunga na Umoja wa Ulaya.

Katika mahojiano na gazeti kabla ya kuwasili Ankara Schroeder amesema Uturuki lazima iboreshe rekodi yake ya haki za binaadamu ambayo haitoweza kutangulika. Baada ya mazungumzo yake na Erdogan kiongozi huyo wa Ujerumani anatazamiwa kuhudhuria mkutano wa uchumi kati ya Ujerumani na Uturuki mjini Istanbul.

Waziri wa uchumi wa Uturuki Ali Babacan amesema ana hofu kwamba Uturuki kujiunga na Umoja wa Ulaya linaweza kuwa suala la uchaguzi nchini Ujerumani hapo mwakani.Wapinzani wa kihafidhina nchini Ujerumani wanasema Uturuki sio tayari kujiunga na Umoja wa Ulaya kwa sababu ya kikwazo cha mageuzi.

Mapema hapo jana Schroeder alitembelea Bosnia ambapo alitowa wito wa kufanyika kwa mazungumzo ya Umoja wa Ulaya ya kuijumuisha nchi hiyo pamoja na kukutana kwa muda mfupi na jamaa za wahanga wa mauaji ya Srebrenica.