ANKARA: Waasi wa Kikurd wameuawa nchini Uturuki
19 Juni 2007Matangazo
Waasi watatu wa Kikurd na mwanajeshi mmoja wa Uturuki,wameuawa katika mapambano mawili mbali mbali,kaskazini mwa Uturuki.Kwa mujibu wa maafisa wa usalama,mwanajeshi huyo aliuawa katika mapigano na waasi wa chama cha Kikurd cha PKK katika mkoa wa Gumushane.Katika mapigano mengine kwenye mkoa wa Erzincan,wanamgambo 3 wa PKK walipigwa risasi na kuuawa na vikosi vya serikali.Mapambano hayo yametokea wakati ambapo serikali inazidi kushinikizwa na umma na majeshi, kuanzisha operesheni ya kijeshi upande wa pili wa mpaka,kaskazini mwa Iraq na iteketeze kambi za PKK.Marekani na Iraq zimesema waziwazi kuwa zinapinga kabisa operesheni ya aina hiyo.