ANKARA: Waasi wa Kikurdi wameuawa Uturuki
29 Mei 2007Matangazo
Uturuki imesema,vikosi vyake vya usalama vimewau waasi 3 wa chama cha PKK cha Wakurdi, kilichopigwa marufuku.Waasi hao waliuawa Jumatatu usiku katika wilaya ya Van baada ya serikali kudokezewa kuwa wataingia Uturuki kutoka nchi ya jirani Iran.Majeshi ya Uturuki yanashiriki katika operesheni kuu dhidi ya PKK kusini-mashariki ya nchi.Zaidi ya watu 37,000 wameuawa,tangu chama cha PKK katika mwaka 1984 kuanzisha mapigano ya kudai utawala wa ndani.