ANKARA:Karzai na Musharraf kukutana nchini Uturuki leo
29 Aprili 2007Matangazo
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan anatarajiwa kuwasili nchini Uturuki leo ambapo atakutana na rais Pervez Musharraf wa Pakistan ili kujadili mbinu za ufanisi za kupambanna na magaidi.
Viongozi hao pia watazungumzia njia za kuratibu mbinu za kuleta amani na utengemavu katika eneo lao.
Marais hao wamekuwa wanalaumiana hivi karibuni juu ya suala la magaidi.