ANKARA:Marekani kuitaka radhi Uturuki
14 Oktoba 2007Marekani imewapeleka Uturuki maafisa wawili wa ngazi za juu serikalini kujaribu kupoza moto mgogoro wa kidiplomasia kati yao.Hatua hii inachukuliwa baada ya kamati ya bunge ya masuala ya kigeni kupigia kura inayoelezea mauaji ya raia wa Armenia nchini Uturuki mwaka 1915-17 wakati wa utawlaa wa Ottoman kuwa ya halaiki.Maafisa hao ni balozi wa zamani wa Marekani nchini Uturuki Eric Edelman pamoja na Naibu Waziri wa mambo ya kigeni wa masuala ya Ulaya Dan Fried walikutaka na Ertugrul naibu waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki.
Lengo la ziara hiyo ni kuitaka Uturuki radhi kwa kupitishwa kwa azimio hilo na kuongeza kuwa Ikulu ya Whitehouse inatia juhudi zote kuizuia kuidhinishwa na bunge zima.Maafisa hao wawili walikuwa ziarani nchini Urusi na Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleeza Rice kabla kufanya ziara hiyo ya ghafla nchini Uturuki.
Uturuki kwa upande wake ilishaionya Marekani kuwa hatua hiyo huenda ikaathiri uhusiano kati ya mataifa hayo mawili vilevile Marekani kupoteza kituo muhimu cha kijeshi nchini humo.Uturuki kwa sasa imemrejesha nyumbani balozi wake wa Marekani.
Kulingana na Armenia yaapata raia wake milioni 1.5 waliuawa katika kipindi cha mwaka 1915-17 katika kampeni ya mateso na kurejeshwa nyumbani kwa nguvu wakati wa utawala wa Ottoman.Uturruki inakiri kuwa Warmenia laki mbili u nusu hadi nusu milioni walipoteza maisha yao aidha idadi hiyohiyo ya raia wake .Hata hivyo inapinga hatua ya kuayaleza mauaji hayo kuwa ya halaiki.