Ardhi inayodaiwa kumilikiwa na Ruto yaibua mzozo
13 Machi 2024Akizungumza kwenye bunge la Seneti, seneta wa Naivasha Tabitha Keroche, amewasilisha ombi la kutaka uchunguzi na ufafanuzi kuhusu kufurushwa kwa watu laki moja, na elfu arobaini kutoka kwenye shamba la Ndabibi lililoko Naivasha.
Mizozo ya ardhi: Kenya yatakiwa kushughulikia sakata la ardhi
"Tunataka kujua sababu ya kuharibiwa kwa makaazi elfu 40,000, kafyu zisizohalali, wizi wa mazao ya mashamba unaofanywa na polisi, wakaazi kufyatuliwa risasi wakiwa nyumbani kwao, vurugu, ubakaji na watu zaidi ya mia moja kukamatwa na kuzuiliwa kinyume na sheria.”
Wiki iliyopita watu 19 walikamatwa na kufikishwa mahakamani katika kaunti ya Nakuru baada ya kuvunja ua kwenye shamba hilo la Ndadidi lenye ukubwa wa eka elfu tano, na kuharibu mali ya mamilioni ya pesa. Wakaazi hao ambao wengi wao ni wakulima wanadai ardhi hiyo ni yao, wengi wao wakiwa wameishi hapo kwa miaka mingi.
"Tunauliza kwani sisi hatuna haki, kuna mama ameshikwa sahizi tunavyoongea, ana Watoto, ni siku tano sasa. Tunauliza ni kwanini hawapelekwi kotini? Na sisi tumeumizwa hata mwenzetu ameumizwa mguu, " alisema David Chege.
Mkaazi mwingine Joshua Manasi naye aliuliza "Mimi ni mmoja wa wale waliopewa hili shamba, nilikuja hapa mwaka 1957. Haya shule imechukuliwa, hospitali imechukuliwa, hata sisi tunashindwa tutatokea wapi?”
Soma: Rais Uhuru aanza kutatua tatizo la ardhi Kenya
Wametishia kufunga shule eneo hilo iwapo mzozo huo hautatatuliwa na wapewe hati miliki ya ardhi. Hata hivyo kwenye baraza la umma lililoandaliwa na viongozi wa eneo hilo, naibu kamishna wa Nakuru Mutua Kisilu amesema hawatasita kuimarisha usalama eneo hilo.
"Wiki hii najua tumekimbizana sana na sio kupenda kwetu, lakini sasa hauwezi kuweka kidole kwa Rais wangu halafu ninyamaze. Watu walisema ati watafunga shule na kuna watu kweli wanajua kuongea mambo hawawezi kweli, unafunga shule ya nani kweli?”
Fuatilia habari hii: Kenya: Wazee wa wamijikenda waandamana
Mbunge wa Naivasha Jayne Kihara amemtambulisha Rais William Ruto kama mmiliki halali wa ardhi hiyo ya Nadabibi. Anasema Rais alinunua ardhi hiyo kihalali kutoka kwa Benjamin Kulei aliyekuwa mwanadiplomasia katika utawala wa Rais mstaafu marehemu Daniel Moi.
"Nimekuja hapa ndio kama kuna shamba ya mtu hapa ambayo Rais amechukua, aje hapa nimpeleke kwa Rais, ndio amuambie mheshimiwa Rais ulichukua shamba langu.”
Hata hivyo, Seneta Tabitha Keroche amelieleza bunge kuwa mwezi Februari mwaka huu mahakama ya Naivasha.