1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoMarekani ya Kusini

Argentina kuandaa duru ya pili ya uchaguzi wa rais

23 Oktoba 2023

Wapigaji kura walikuwa na chaguo kati ya wagombea watatu wakuu wakiwemo mwanauchumi Javier Milei, waziri wa uchumi Sergio Massa na mhafidhina Patricia Bullrich.

https://p.dw.com/p/4XsqZ
Kombobild Javier Milei und Sergio Massa
Wagombea urais wa Argentina, Javier Milei, kushoto, na Sergio Massa, kulia.Picha: Agustin Marcarian/AP/picture alliance/Tomas Cuesta/Getty Images

Waziri wa uchumi wa Argentina Sergio Massa na mgombea anayepinga utawala Javier Milei watapambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais kwa mujibu wa matokeo ya awali ya uchaguzi uliofanyika jana Jumapili. Kwa mujibu wa katibu mkuu wa afisi ya rais, Massa amepata asilimia 35.9 ya kura na Milei asilimia 30.51 baada ya asilimia 76.12 ya kura kuhesabiwa.

Raia wa Argentina walijitokeza kwenye vituo vya kupigia kura jana Jumapili kushiriki uchaguzi huku nchi hiyo ikikabiliwa na mdororo mbaya kabisa wa uchumi katika kipindi cha miongo miwili na ghadhabu ikiongezeka dhidi ya viongozi.