Armenia na Azerbaijan zakubaliana msingi wa mkataba wa amani
18 Novemba 2023Matangazo
Haya yamesemwa na Waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan.
Kulingana na shirika la habari la Urusi la TASS, Pashinyan amesema kuna hatua zilizopigwa katika mazungumzo yanayoendelea kuhusiana na mkataba wa amani, ingawa amenukuliwa akisema kuwa nchi hizo mbili aghalabu huwa na wakati mgumu kukubaliana kuhusu baadhi ya mambo.
Armenia na Azerbaijan zimezozana kwa miongo kadhaa sasa kutokana na eneo la Nagorno-Karabakh ambalo majeshi ya Azerbaijan yalichukua tena udhibiti wake mwezi Septemba na kupelekea idadi kubwa ya Waarmenia kuondoka.