SiasaAsia
Armenia na Azerbaijan zashambuliana
13 Mei 2023Matangazo
Inaarifiwa mapigano hayo yamesabababisha kila upande kupoteza askari wake mmoja. Uhasama huo unashuhudiwa kuelekea mkutano uliopangwa siku ya Jumapili mjini Brussels kati ya waziri mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan na rais Ilham Aliyev wa Azerbaijan. Mkutano huo unalenga kutafuta suluhu ya kudumu ya mvutano wa muda mrefu kati ya mataifa hayo juu ya eneo la Nagorno -Karabakh.
Kwa miongo mitatu mataifa hayo yaliyokuwa sehemu ya Dola ya Kisovieti yanapigana kuwania eneo hilo lenye wakaazi wengi wenye asili ya Armenia lakini linatambulika kama sehemu ya Azerbaijan.