SiasaAsia
ASEAN yatiwa wasiwasi na mapigano Myanmar
19 Aprili 2024Matangazo
Kauli hiyo imetolewa baada ya kutokea hivi karibuni kwa mapigano ya kuwania kituo muhimu cha shughuli za biashara kilichoko katika eneo la mpaka wa Thailand.
Mawaziri wa mambo wa ya nje wa Jumuiya hiyo wamezitolea mwito pande zote za mzozo huo kusitisha vurugu nchini Myanmar ambako vita vimekuwa vikishuhudiwa tangu jeshi lilipotwaa madaraka kwa nguvu mwezi Februari mwaka 2021.
Soma zaidi: Thailand yaanza kupeleka misaada nchini Myanmar
Wiki iliyopita jeshi lililazimika kuondowa vikosi vyake katika kituo cha biashara cha Myawaddy baada ya siku kadhaa za mapambano na kundi la wanamgambo wa kabila la wachache linaloitwa Karen National Union (KNU) wanaoshirikiana na makundi mengine yanayolipinga jeshi.