Ni miongoni mwa watu wasiojulikana sana katika harakati za uhuru barani Afrika, lakini Louis Rwagasore ni mtu aliyeiongoza Burundi kuelekea uhuru wake bila ya ghasia. Hata hivyo hakufaidi matunda ya juhudi zake, kwani aliuawa muda mfupi baada ya Burundi kutangaza uhuru wake. Louis Rwagasore ambaye hakudumu katika wadhifa wa waziri mkuu , alikuwa rafiki wa Patrice Lumumba na Julius Nyerere.