Assange aachiwa huru kwa dhamana
25 Juni 2024WikiLeaks imesema Assange aliachiliwa huru kwa dhamana kutoka gerezani mjini London, alikokuwa amezuiliwa kwa miaka mitano wakati akipigana kuepuka kupelekwa nchini Marekani, ambayo ilitaka kumfungulia mashtaka kwa kuvujisha siri za kijeshi. Mke wa mtuhumiwa huyo, Stella Assange anasema atamuombea msamaha mumewe.
"Kwa uhakika, ninamaanisha nadhani kwamba hatua sahihi kwa serikali ya Marekani inapaswa kufuta kesi hiyo kabisa, ni wazi tutakuwa tunatafuta msamaha lakini ukweli kwamba kuna shitaka la hatia chini ya Sheria ya Ujasusi na kufichua habari za Ulinzi wa Kitaifa ni wazi kuwa ni wasiwasi mkubwa kwa waandishi wa habari na wanaonadika habari za usalama wa taifa kwa ujumla," alisema Stella Assange.
Julian Assange akubaliwa kupinga hukumu ya kuhamishwa Marekani
Jana Jumatatu alisafiri kwa ndege kutoka London kwenda Visiwa vya Mariana Kaskazini, eneo la Marekani ambapo atakiri shtaka moja la kula njama ya kupata na kusambaza habari za ulinzi wa kitaifa, kwa mujibu wa hati ya mahakama.