AU yaendelea kuukamilisha mkataba wa biashara huru
5 Julai 2019Matangazo
Mataifa 55 ya Umoja huo yatakusanyika mwishoni mwa juma katika mkutano wa kilele nchini Niger yakijaribu kuondoa ushuru wa biashara miongoni mwa nchi wanachama.
Kundi linalounga mkono mkataba huo huru wa Afrika (AfCFTA) wanaamini kwa kufanya hivyo, biashara baina ya mataifa ya Afrika itaimarika.
Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat, alisema jana mjini Niamey kuwa hayo ni mafanikio makubwa na yanayoweza kuelezewa kama historia.
Nigeria imesema itatia saini mkataba huo baada ya kugoma kwa muda mrefu.
Mazungumzo kuhusu biashara huru yalianza mwaka 2002 na kuungwa mkono na mataifa mengi huku Benin na Eritrea zikiwa za mwisho kutia saini.