Azerbaijan yataka Armenia kuondosha wanajeshi N. Karabkh
19 Septemba 2023Wizara ya ulinzi ya Azerbaijan imesema oparesheni hiyo ilianza saa chache baada ya wanajeshi wanne na raia wawili kufa katika mripuko wa mabomu ya kutegwa ardhini huko Nagorno-Karabakh.
Hata hivyo, Azerbaijan imesema imefungua njia za kiutu kwa wasio wapiganaji katika eneo hilo ili kukimbia mapigano yaliyoanza.
Soma zaidi: Nagorno-Karabakh yamchagua rais mpya
Urusi imezitaka Azerbaijan na Armenia kuheshimu makubaliano ya kusitisha vita ya Karabakh na kukomesha umwagaji damu na kufuata demokrasia.
Armenia imeishutumu Azerbaijan kwa kujaribu kuanzisha kampeni ya mauaji ya kikabila huko Karabakh.
Umoja wa Ulaya umelaani kuongezeka kwa mvutano wa kijeshi katika eneo linalozozaniwa la Nagorno-Karabakh, na umeitaka Azerbaijan kusitisha mara moja operesheni yake.