1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Azerbaijan:Wanajeshi 100 wamekufa mzozo wa Nagorno Karabakh

27 Septemba 2023

Azerbaijan imesema wanajeshi 192 na raia mmoja waliuwawa kwenye operesheni yake ya kijeshi ya wiki iliyopita ya kuwania udhibiti wa jimbo la Nagorno Karabkah dhidi ya wapiganaji wenye asili ya Armenia.

https://p.dw.com/p/4WrFd
Askari jeshi wa Armenia akiwa katika jukumu lake la kulinda usalama
Askari jeshi wa Armenia akiwa katika jukumu lake la kulinda usalamaPicha: Karen Minasyan/AFP/Getty Images

Takwimu hizo zimetolewa leo na wizara ya afya ya nchi hiyo ambayo pia imesema wanajeshi wengine 500 walijeruhiwa kwenye makabiliano hayo yaliyomalizika kwa ahadi ya waasi wa Kiarmenia kuweka chini silaha. 

Soma pia:'Madai ya safishasafisha ya kikabila dhidi ya Azerbaijana ni tusi kwa taifa hilo, serikali yasema

Wakati hayo yakiarifiwa, maelfu ya Waarmenia wameendelea kulikimbia jimbo la Nagorno Karabakh wakihofia usalama baada ya Azerbaijan kuchukua udhibiti kamili wa eneo hilo ambalo limekuwa chanzo cha mzozo kati yake na Armenia kwa zaidi ya miaka 30.

Tangu wiki iliyopita zaidi ya Waarmenia 28,000 kati ya 120,000walio wakaazi wa jimbo la Karabakh wamevuta mpaka na kuingia Armenia kukimbia kile wengi wamekitaja kuwa wasiwasi wa Azerbaijan kulipa kisasi kwa kuwafanyia vitendo vya kikatili.