Kenya kuiomba China mkopo wa dola bilioni moja
6 Oktoba 2023Naibu wa rais Rutto, Rigathi Gachagua amesema hayo leo na kuongeza kuwa Ruto atatoa ombi hilo wakati wa ziara yake nchini China baadaye mwezi huu.
Gachagua amesema wakipata dola bilioni moja, basi wawalipa wanakandarasi madeni yao ili waweze kuendelea na ujenzi wa miradi.
Mikopo ya China kwa Kenya ambayo hadi sasa ni zaidi ya dola bilioni nane, ilitumika ya utawala wa rais wa zamani Uhuru Kenyatta kujenga miundo mbinu kama barabara. Lakini miradi mingi ilikwama baada ya waliopewa kandarasi kuondoka kwa sababu ya malimbikizi ambayo hayajalipwa.
Mpango huo wa Rais Ruto unakwenda kinyume na msimamo wake kuhusu madeni ya China hasa wakati walipokuwa wakifanya kampeni kuingia madarakani ambapo muungano wake unaotawala sasa ulikosoa ukopeshaji uliokuwa ukifanywa na utawala wa mtangulizi wake