1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bado hakuna makubaliano ya Ujerumani kupeleka vifaru Ukraine

20 Januari 2023

Waziri mpya wa Ulinzi wa Ujerumani amesema hafahamu kuhusu kuwepo mpango unaoitaka kupeleka vifaru vya kijeshi nchini Ukraine sambamba na Marekani.

https://p.dw.com/p/4MUpV
Ramstein-Treffen zum Krieg in der Ukraine | Verteidigungsminister Pistorius
Picha: dpa

Serikali ya Ujerumani mpaka sasa haijaidhinisha usafirishaji wa vifaru vya kivita vilivyotengenezwa Ujerumani chapa Leopard nchini Ukraine,na vyanzo vinasema  serikali mjini Berlin itachukua hatua hiyo ikiwa Marekani itakubali kutuma Ukraine vifaru vyake vya kivita chapa Abrams. Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky amesema serikali yake inatarajiwa kuona maamuzi thabiti kutoka kwa viongozi wa jumuiya ya kujihami ya NATO na nchi nyingine wanaokutana leo kujadili mpango wa kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Ukraine kupambana na vikosi vya Urusi. Akifungua mkutano katika kambi ya kijeshi ya Ramstein,waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin amezitolea mwito nchi kutoa mchango zaidi kuisaidia Ukraine.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW