1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock aiangazia Sudan katika ziara ya Afrika Mashariki

26 Januari 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock aliwasili nchini Kenya Alhamisi na kukutana na rais wa nchi hiyo William Ruto, katika ziara ambayo italenga zaidi mzozo wa Sudan

https://p.dw.com/p/4bguK
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ahudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje mjini Brussels, Januari 22, 2024
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena BaerbockPicha: Thomas Imo/photothek/picture alliance

Rais Ruto alimpokea mwanadiplomasia huyo mkuu wa Ujerumani katika moja ya makazi ya nchi yake nchini humo, Sagana Lodge.

Soma pia:Baerbock afuta ziara ya Djibouti

Mkutano huo na Ruto huenda pia ukalenga mapambano mabaya ya madaraka nchini Sudan na athari zake kwa eneo hilo.

Baerbock atoa wito wa juhudi zaidi za suluhisho kwa mzozo wa Sudan

Mwanzoni mwa ziara yake, Baerbock tayari alikuwa ametoa wito wa kuongezwa kwa juhudi za kutafuta suluhisho la mazungumzo nchini Sudan.

Soma pia:Baerbock atua Jeddah kwa dharura baada ya ndege yake kukosa kibali cha kutua Djibouti

Baerbock amesema kuwa nchi katika kanda hiyo, Jumuiya ya Ushirikiano wa Nchi za Pembe ya Afrika IGAD na Umoja wa Afrika zinatekeleza jukumu muhimu katika juhudi za upatanishi za kimataifa.

Soma pia:Baerbock ahimiza 'shinikizo' Sudan

Mbali na Djibouti, IGAD inazijumuisha pia Eritrea, Ethiopia, Somalia,

Kenya, Sudan, Sudan Kusini na Uganda. Sudan imesitisha uanachama wake.

Kundi hilo linatafuta mazungumzo ya moja kwa moja kwa ajili ya kusitisha mapigano nchini Sudan.