1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUjerumani

Baerbock aitolea wito Israel kusitisha miradi ya makaazi

6 Septemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameitolea wito Israel kusitisha miradi ya makaazi ya walowezi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi, wakati wa mazungumzo mjini Tel Aviv mapema leo.

https://p.dw.com/p/4kMug
Israel Tel Aviv | Baerbock na Katz
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Israel Katz, kulia, akisalimiana na mwenzake wa Ujerumani Annalena Baerbock kabla ya mkutano wao mjini Tel AvivPicha: Leo Correa/AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ameitolea wito Israel kusitisha miradi ya makaazi ya walowezi kwenye eneo la Ukingo wa Magharibi, wakati wa mazungumzo mjini Tel Aviv mapema leo.

"Mwisho wa wiki umedhihirisha kwamba hatua za kijeshi pekee sio suluhu katika vita vya Gaza. Wiki iliyopita tuliona kampeni ya kijeshi inahatarisha maisha ya mateka. Ni wazi kabisa, kuna haja ya kusitisha vita. Kuna haja ya kusitisha mapigano sasa."

Soma pia:  Ujerumani yataka mzozo wa Gaza umalizike

Kabla ya mazungumzo haya, Baerbock alizizuru Saudi Arabia na Jordan katika ziara yake ya kuhamasisha usitishwaji mapigano, kurejeshwa mateka na misaada zaidi kwa Gaza.

Katika hatua nyingine, vikosi vya Israel vimeonekana kuondoka katika mji wa Jenin na makambi mawili ya wakimbizi katika eneo inalolikalia kimabavu la Ukingo wa Magharibi baada ya operesheni kubwa ya kijeshi ya karibu siku 10 iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa.