1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Baerbock akamilisha ziara ya siku nne Iraq

10 Machi 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock, leo amekamilisha ziara yake ya siku nne nchini Iraq, kwa kuutembelea ujumbe wa mafunzo wa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, mjini Erbil.

https://p.dw.com/p/4OWYB
Annalena Baerbock im Irak
Picha: Hadi Mizban/AP/picture alliance

Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alikuwa mjini Erbil, kaskazini mwa Iraq, ili kujua zaidi kuhusu ujumbe huo ulioko nchini humo.

Katika kambi ya Stephan, mwanasiasa huyo kutoka chama cha watetezi wa mazingira, alioneshwa gari la wagonjwa lenye uwezo wa kupita kila mahaka, ambalo linaweza kusafirisha majeruhi.

Ameoneshwa pia silaha yenye uwezo wa kutatiza mashambulizi ya ndege za adui zisizo na rubani. Jana  Baerbock  alitembelea maeneo yalioshuhudia ukatili wa kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu, IS katika mkoa wa Sinjar, karibu na mpaka na Syria.