1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock atazama mazoezi ya kupambana na ugaidi Ivory Coast

17 Julai 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock alitazama mazoezi ya kukabiliana na ugaidi nchini Ivory Coast, yenye lengo la kupambana na kitisho cha ugaidi kuingia katika mataifa mengine kutoka kanda ya Sahel.

https://p.dw.com/p/4iPbz
Baerbock yupi Ivory Coast
Baerbock atazama mazoezi ya kupambana na ugaidi Ivory CoastPicha: Rosalia Romaniec/DW

Baerbock alikuwa katika ziara yake ya Afrika Magharibi ambapo aliarifiwa kuhusu mazoezi yanayo jumuisha jeshi, polisi na vikosi vya usalama vya kiraia katika chuo cha kimataifa cha Jacqueville. 

Ujerumani inaisaidia Ivory Coast katika ufadhili wa miundo mbinu ya chuo hicho cha kimataifa cha mafunzo ya kijeshi kwa kutoa dola milioni 2.7.

Ujerumani haiwezi tena kushirikiana na Niger kijeshi

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Baerbock pia amesema Ujerumani haiwezi tena kushirikiana kijeshi na taifa jirani la Niger kutokana na ukosefu wa "imani" katika uhusiano na utawala wa kijeshi wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Hii ni baada ya Ujerumani mnamo Julai 6 kutangaza kwamba itamaliza operesheni za kijeshi nchini Niger na kuwaondoa wanajeshi wake waliosalia ifikapo Agosti 31.