Baerbock aunga mkono msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine
22 Mei 2024Matangazo
Mwanadiplomasia huyo wa Ujerumani amesema anaunga mkono wito huo pamoja na ule wa waziri wa ndani wa taifa hilo akisema kwa sasa wanachohitaji ni bajeti ya masuala ya Usalama.
Gazeti la kila Jumapili la Bild liliripoti kuwa Pistorius anapanga kuomba msaada wa ziada wa dola bilioni 4.3 kwa usaidizi wa kijeshi wa Ukraine kwa mwaka huu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo tayari Ujerumani imetoa dola bilioni 7.1 kwa Ukraine kwa mwaka 2024.
Ripoti ya gazeti ya Bild imesema tayari pesa hizo zimeshatumika na kilichobakia ni milioni 300 ya manunuzi ya silaha nyengine.