Baerbock kuhudhuria ufunguzi wa kiwanda cha chanjo Rwanda
17 Desemba 2023Kwa mujibu wa wizara ya maendeleo ya Ujerumani, serikali mjini Berlin inaunga mkono inaunga mkono juhudi za utengenezaji endelevu wa chanjo hiyo barani Afrika kulisaidia kujiandaa kwa ajili ya kukabiliana na miripuko ya siku za baadae.
Kampuni ya utengenezaji dawa ya BioNtech yenye makao yake mjini Mainz inapanga kutengeneza chanjo hiyo kwa teknolojia ya mRNA katika kiwanda hicho cha Kigali kuanzia mwaka Ujao.
Kuna uwezekano pia wa chanjo nyingine kama hizo dhidi ya Malaria na kifua Kikuuu kutengezwa katika kiwanda hicho katika miaka ya baadae endapo kibali cha kuidhinisha hatua hiyo kitatolewa.
Ujerumani inachangia zaidi ya Yuro Milioni 550 katika kuusaidia Umoja wa Afrika kufikia lengo lake la kutengeneza asilimia 60 ya chanjo zinazotumika barani humo kufikia mwaka 2040.
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Rwanda Vincent Biruta mjini Kigali na kutembelea makumbusho ya wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.