BAGHDAD Ziara ya waziri wa Mambo ya nje wa Marekani nchini Iraq
16 Mei 2005Matangazo
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice Katika ziara yake ya ghafla nchini Iraq amekutana na waziri mkuu wa nchi hiyo Ibrahim Al Jafaari rais Jalal Talabani na maafisa wengine wa serikali na kuahidi kwamba Marekani itaendelea kuiunga mkono serikali mpya ya Iraq.
.
Bibi Rice akiwa kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu wa Marekani kuwahi kuitembelea Iraq tangu kuundwa kwa serikali mpya ya Iraq mapema mwezi huu, aliiwasili kwa ndege ya kijeshi kutoka nchini Qatar hadi kaskazini mwa mji wa kikurdi wa Salahuddin akiwa chini ya ulinzi mkali.
Bibi Rice pia amewataka wananchi wa Iraq kuwa na subira na serikali mpya katika kupambana na waasi wanaondeleza mashambulizi nchini Humo.