1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

BAGHDAD:Wanajeshi wa Uturuki wapelekwa kwenye mpaka kaskazini ya Iraq

10 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBkK

Uturuki imeweka wanajeshi kiasi laki moja na 40 elfu katika mpaka wake na kaskazini mwa Iraq.Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Iraq Hoshyar Zabari jeshi la Uturuki linasubiri kupata idhini kutoka serikali ya Iraq kuanzisha opresheni dhidi ya waasi wa kikurdistan wa chama cha PKK ambao wako katika eneo la kaskazini mwa Iraq.

Msemaji wa ikulu ya Marekani amesema Marekani ina wasiwasi kama Uturuki juu ya wapiganaji hao wakikurdi nchini Iraq lakini imeitolea mwito serikali ya mjini Ankara kutochukua hatua za kijeshi katika mpaka wa eneo la kusini kuingia Iraq. Wakati huohuo maafisa wa Ikulu ya Marekani wakitafakari iwapo rais Bush anapaswa kutangaza kuyaondoa majeshi yake nchini Iraq rais Bush amesema hawezi kufikia uamuzi kama huo licha ya kupata shinikizo zaidi kutoka chama chake cha Republican kubadili mwelekeo juu ya vita nchini.Bush amesema kuondoka nchini humo kabla ya kutimiza lengo lao kutakuwa ni kosa kubwa.

Viongozi nchini Iraq wameonya kwamba kuondoka mapema wanajeshi wa Marekani nchini humo huenda kukaitumbukiza kwenye vita kamili vya wenyewe kwa wenyewe