1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bahamas kuungana na Kenya katika amani ya Haiti

2 Agosti 2023

Bahamas yaipongeza Kenya kushiriki katika juhudi za amani za Haiti huku ikitoa ahadi ya kujumuisha askari wake 150 katika juhudi hiyo.

https://p.dw.com/p/4Ugb4
Haiti | Ermordung Präsident Jovenel Moise
Picha: Valerie AFP/Getty Images

Serikali ya Bahamas imeupongeza uamuzi wa Kenya kuongoza kikosi cha kimataifa nchini Haiti huku mamlaka ya kisiwa hicho ikiahidi kutoa askari 150 ili kuunga mkono juhudi za kuimarisha usalama iwapo Umoja wa Mataifa utaidhinisha kikosi hicho cha kulinda amani. Tangazo hilo la wizara ya mambo ya nje ya Bahamas linafuatia ombi lililotolewa siku ya Jumatatu na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kwamba Bahamas iungane na Kenya katika juhudi za kulinda amani. Wiki iliyopita, Kenya ilieleza utayari wake wa kupeleka maafisa 1,000 wa polisi nchini Haiti ili kuisaidia nchi hiyo kupambana na vurugu za magenge. Bahamas imeunga mkono kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Mutua, aliyefafanua kuwa juhudi za kuimarisha usalama huko Haiti ni moja ya fursa ya "kusimama na watu wenye asili ya Kiafrika duniani kote."