1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bahrain yapendekeza mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati

16 Mei 2024

Bahrain imetoa wito wa kuandaliwa kwa mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliogubikiwa na suala la vita vya Israel na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4fwq6
Hamad bin Isa Al Khalifa
Mfalme wa Bahrain Hamad bin Isa Al KhalifaPicha: Royal Court of Saudi Arabia/AA/picture alliance

Bahrain imetoa wito wa kuandaliwa kwa mkutano wa amani wa Mashariki ya Kati wakati wa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu uliogubikiwa na suala la vita vya Israel na kundi la Hamas.

Akihutubia mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na mjini Manama, Mfalme Hamad bin Isa Al Khalifa ametoa wito wa kuitishwa kongamano la kimataifa la amani Mashariki ya Kati, pamoja na kuungwa mkono hatua ya kulitambuwa kikamilifu Dola la Palestina na kukubali uanachama wake katika Umoja wa Mataifa.

Soma: Mazungumzo ya kujadili vita vya Gaza kufanyika Saudi Arabia

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas aliuambia mkutano huo kwamba wapinzani wake wa kisiasa - kundi la Hamas waliipa Israel kisingizio cha kuanzisha vita dhidi ya Gaza.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema njia pekee na ya kudumu ya kumaliza mzunguko wa ghasia na ukosefu wa utulivu ni kupitia suluhisho la serikali mbili.