Bale: "Ukame wa mabao" haunishtui
11 Juni 2021Nahodha wa timu ya Wales Gareth Bale amesema hashtushwi na ukame wake wa mabao katika mechi za kimataifa saa chache kabla ya mechi ya ufunguzi dhidi ya Uswisi. Soma zaidi Lijue kundi C la michuano ya Euro 2020
Mara ya mwisho kwa Bale kuifungia Wales ilikuwa Oktoba 2019 dhidi ya Croatia lakini amefanikiwa kuchangia katika mabao manne katika mechi saba alizojumuishwa.
Hana wasiwasi
"Haijalishi. Nimefanya usaidizi. Bado ninachangia. Sina wasiwasi, kama nafasi itatokea kupata bao, nitaitumia," alisema Bale.
Siku ya Jumamosi Wales itacheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Switzerland.
Mshambuliaji huyo wa Real Madrid, ambaye alitumia msimu uliopita kwa mkopo huko Tottenham, amefunga mabao 33 katika mechi 92 za kimataifa tangu 2006 lakini katika mechi 11 amekuwa na ukame. Bale huenda akakamilisha maisha ya soka Madrid
"Sio mwisho wa ulimwengu. Ikiwa hafungi anawasilisha mabao, muhimu asaidie kuunda mabao, anafanya hivyo." alisema kocha wa Wales, Robert Page.
AFP