1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baraza la katiba Msumbiji yathibitsiha ushindi Daniel Chapo

23 Desemba 2024

Baraza la Katiba la Msumbiji limeidhinisha ushindi wa chama tawala cha Frelimo katika uchaguzi wa rais wa Oktoba 9 ambao umezua maandamano makubwa ya makundi ya upinzani makundi ambayo yanasema kura zilichakachuliwa.

https://p.dw.com/p/4oWee
Mosambik Daniel Chapo
Mgombea urais wa chama tawala cha Front for the Liberation of Mozambique, akiinua kidole chake baada ya kupiga kura yake katika uchaguzi wa rais na wabunge.Picha: AP/dpa/picture alliance

 

Baraza la Katiba ndilo lenye uamuzi wa mwisho kuhusu mchakato wa uchaguzi na uamuzi wake huenda ukachochea zaidi maandamano katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika yenye karibu watu milioni 35. Kiongozi wa upinzani ameapa kuendeleza "vurumai" ikwapo chama tawala kingethibitishwa kuwa mshindi katikati ya mzozo ambao tayari umegharimu maisha ya watu 130. Mwanasiasa wa Frelimo, Daniel Chapo sasa anatarajiwa kuchukua nafasi ya Rais Filipe Nyusi ambaye muhula wake wa pili unamalizika Januari 15.